Marapa Quavo Huncho na Take Off kutoka Marekani wamemkataa aliyekuwa shemeji yao Cardi B ambaye ni Baby Mama wa Offset aliyekuwa anaunda kundi la Migos.
Wawili hao baada ya kuulizwa kwenye mahojiano na Drink Champs kuwa wapo upande upi kati ya Cardi B na Nick Minaji Take Off Bila kusita alimtaja Nicki Minaj.
Kauli hii imezua mijadala kwa mashabiki wengi wakidai kuwa jamaa wameamua kumkomesha Cardi B maksudi kufuatia kuvunjika kwa kundi la Migos kwani inaaminika kuwa Cardi B ndiye alimshawishi kimapenzi Mume wake Offset ajiondoe kwenye kundi la Migos.