You are currently viewing MARIOO AMUUNGA MKONO ERIC OMONDI

MARIOO AMUUNGA MKONO ERIC OMONDI

Kufuatia mjadala ambao anauendeleza mchekeshaji Eric Omondi akipaza sauti juu ya wasanii wa Kenya kutotendewa haki na waandaaji wa matamasha ya muziki, Staa wa muziki wa Bongofleva Marioo ameamua naye kuuvunja ukimya.

Kwa asilimia mia moja Marioo ameziunga mkono harakati za Eric Omondi, ameamua kufunguka ya moyoni kwa kuisemea tasnia ya muziki Bongofleva  ambapo amedai waandaaji wa matamasha ya muziki wamekuwa wakiwapa nafasi ya kipekee wasanii wa nje huku wasanii wa ndani wakichukuliwa poa tu.

Hitmaker huyo wa “Beer Tamu” amewachana pia wasanii wakubwa kutoka Tanzania ambao wamekuwa wakifanya Collabo na wasanii wachanga kutoka Nigeria & Afrika Kusini na kukataa kuwapa mashavu (support) wasanii wa ndani ili kukuza sana Tanzania kwa ujumla.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke