Staa wa muziki wa Bongofleva, Marioo ni kama tayari ameikamilisha Album yake mpya ambayo huenda ikaingia sokoni hivi karibuni.
Kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram Mkali huyo wa ngoma ya Dear Ex amesema ngoma zilizopo kwenye album yake hiyo ni za moto lakini pia kuna nyimbo ambazo zimebaki na anashindwa aziweke wapi.
“Yaani kwenye albamu mangoma yamejaa halafu yote moto, halafu bado nipo na mawe mengine, hata sijui nayafanyia nini na bado nipo na mood ya kurekodi” amesema Marioo.
Kwenye andiko lake hilo ameishia kwa kusema anafikiria kuwabariki mashabiki zake na zawadi ambayo walimwengu wametafsiri huenda msanii huyo ana mpango wa kuachia EP kabla ya Album.
Utakumbuka juzi kati Marioo alitudokezea kuwa ngoma zake kama Mi Amor, Naogopa na Dear EX zitakuwepo kwenye albamu yake mpya.