Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Marioo hataki kuibeba bendera ya Taifa lake pekee yake kuipeleka duniani, anataka umoja wa wasanii wote kwa pamoja.
Kupitia insta story yake, mkali huyo kwa sasa kwenye Muziki wa Bongo Fleva, ametoa angalizo kwa wasanii wenzake kuwa waendelee kujitahidi kuachia kazi kali kwani na yeye atahakikisha baada ya uzinduzi wa Album yake “The Kid You Know” Januari 28 mwaka huu itakuwa ni mwendo wa kuachia kazi kali tu.
Hitmaker huyo wa “Mi Amor” amesema lengo lake ni kuupeleka muziki wa Bongo Fleva kote duniani.