Staa wa Muziki wa Bongofleva Marioo ambaye kwa sasa anafanya poa na singo yake “Mi Amor” ameamua kutoa somo kwa wasanii chipukizi.
Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Marioo amewaambia wasanii hao kuwa wanapohitaji kutoa wimbo wahakikishe wimbo husika unakuwa mkali kuliko nyimbo zilizopo masikioni mwa watu.
Mbali na hayo, ameendelea kutusanua kuhusu ujio wa album yake mpya kwa kusema kwamba album yake itaitwa “The Boy You Know” na itaingia sokoni kabla ya mwaka huu haujakamilika.
Utakumbuka usiku wa kuamkia Aprili 3 kwenye hafla ya ugawaji wa tuzo za Tanzania Music Awards Marioo alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Bongofleva na Wimbo Bora wa Bongo Fleva wa Mwaka kupitia ngoma yake ya “Beer Tamu”