You are currently viewing MARIOO KUACHIA ALBUM NA EP HIVI KARIBUNI

MARIOO KUACHIA ALBUM NA EP HIVI KARIBUNI

Hitmaker wa wimbo ‘Beer Tamu’ msanii Marioo, ameweka wazi ujio wa EP (Extended Playlist) na album yake mpya siku za hivi karibuni.

Marioo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya walioliteka anga la Bongofleva ndani ya muda mfupi, ameeleza kuwa amerekodi ngoma nyingi na bado anatamani kurekodi, akidai nyingine zitaoza ndani. Hivyo ni wakati wa kuachia EP na Album.

“Nimerekodi ngoma nyingi sana halafu zote kali yani mpaka nadata, halafu hizi ngoma zitaoza humu ndani na bado natamani kurekodi ngoma mpya, Aisee EP & ALBUM Is Coming” – ameandika Marioo kupitia insta story yake.

Marioo ambaye jina lake kamili ni Omari Mwanga amekuwa na mwenendo mzuri wa kuachia kazi kali mwaka huu, tutarajie maajabu mengine kutoka kwenye EP na Album yake mpya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke