You are currently viewing MARO ATANGAZA UJIO MPYA BAADA YA UKIMYA WA MUDA MREFU.

MARO ATANGAZA UJIO MPYA BAADA YA UKIMYA WA MUDA MREFU.

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda Maro ametangaza kurejea tena kweny tasnia ya muziki baada ya kuchukua mapumziko mwaka wa 2019.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Maro amesema ataanza tena biashara mwezi Disemba mwaka huu ambapo ameweka wazi mpango wa kuanza kuwaandikia wasanii nyimbo lakini pia kufanya kollabo na wasanii wanaofanya vizuri nchini Uganda.

“Muziki ni biashara yangu kwa hiyo nafungua tena. Na pia naandika nyimbo kwa mtu yeyote ambaye yuko serious kwenye game, serious tayari ana namba yangu! Sheria na masharti yatatumika ingawa. Bado nitashirikiana na nyota wanaochipukia ambao nitawaona wakifanya poa kwenye muziki wao na tena najua wana nambari yangu na wanipige pindi watakapoona huu ujumbe. Wacha tukuze muziki wetu, “ameandika Maro kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyo, baada ya ujio huo Maro ameahidi kuachia kazi mfululizo bila kupoa kutokana na kazi nyingi alizoziandaa wakati wa ukimya wake

Ikumbukwe baada ya kuacha muziki kwa takriban miaka miwili iliyopita, Maro alihamia nchini Ujerumani ambako amekuwa akiishi na mpenzi wake mwenye asili ya mzungu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke