You are currently viewing MARTHA MUKISA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU UGOMVI WAKE NA EDDY YAAWE

MARTHA MUKISA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU UGOMVI WAKE NA EDDY YAAWE

Mwanamuziki chipukizi nchini uganda Martha Mukisa amevunja kimya chake juu ya ugomvi unaoendelea kati yake na Eddy Yaawe kuhusu umiliki wa wimbo wao uitwao “Neteze”

Katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda, mwimbaji huyo amefichua kwamba walikesha usiku kucha katika studio za Dream zinazomilikiwa na Eddy Yaawe wakirekodi wimbo wao mpya “Neteze”.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Busy” ameeleza kuwa walirekodi wimbo huo siku mbili mfululizo huku wakilala studio.

“Nilienda nyumbani kwake Kireka kisha tukafunga safari hadi kwenye studio zake. Tulianza kurekodi na kulala huko na siku iliyofuata tulitofautiana sana kuhusu jina la wimbo,” alisema.

Martha Mukisa amesema bado anamshukuru Eddy Yaawe kwa ushirikiano huo licha ya tofauti zilizojitokeza kutokana na hakimiliki ya wimbo huo.

Utakumbuka wimbo wa “Neteze” ambao ulikuwa umepakiwa kwenye akaunti ya Youtube ya Martha Mukisa ulifutwa na Eddy Yawe kutokana na masuala ya hakimiliki baada ya kutoelewa na uongozi wa msanii huyo kuhusu ishu ya kugawa mirahaba.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke