Hitmaker wa ngoma ya “Chokoza”, Msanii Marya amefunguka na kudai kuwa kuna kipindi alitaka kujitoa uhai akiwa ana ujazito wa mtoto wake wa kwanza.
Katika mahojiano yake na Munga Eve, Marya amesema mawazo ya kutaka kujiua ilikuja baada ya kupatwa na msongo wa mawazo, uhusiano wake na baba wa mtoto wake ulipoanza kuyumba akiwa na mimba ya miezi mitano.
Mrembo huyo amesema ilikuwa na wakati mgumu sana kudhibiti msongo wa mawazo aliyokuwa nayo kipindi hicho ila mwisho alifanikiwa kujitoa katika hali hiyo baada ya kuacha kila kitu na kuanza kujifikiria kwanza kama njia ya kujitibu.
Mbali na hayo amesema anajuta kutumia vibaya pesa alizokuwa anaingiza kupitia muziki wake kipindi ambacho alikuwa na jina kubwa kwenye tasnia ya muziki nchini.
Utakumbuka Marya ambaye alikuwa chini lebo ya muziki ya Ogopa Deejays alikuwa moja kati ya wasanii wakike waliosumbua sana kwenye chati mbali mbali za muziki nchini kupitia ngoma kama Sishiki Simu,Chokoza na nyingine nyingi.