You are currently viewing MASAUTI AFUNGUKA KUFUKUZWA NA PROMOTA JUKWAANI MOMBASA

MASAUTI AFUNGUKA KUFUKUZWA NA PROMOTA JUKWAANI MOMBASA

Staa wa muziki nchini Masauti amevunja kimya chake baada ya kudaiwa kuwa alifukuzwa jukwaani kwenye tamasha la muziki lilofanyika Mombasa wikiendi iliyopita.

Kupitia waraka aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa instagram Masauti amesema masaibu yake yalitokana na promota wa tamasha hilo huku akiwataka mashabiki kutomulaumu mbosso kwani hakuwa mhusika mkuu wa show hiyo.

“Sijataka kuongelea issue ya show ya Mombasa lakini pia nimeona nivunje ukimya ili kuepuka unafki. Najua mashabiki zangu wanahofu kutaka kujua what exactly happened ndio singependelea mtu atumie jina langu kuelezea my side of the story. Nataka niwaombe tu kwanza tukio hili lilitokea lisitumike kumharibia rafiki yangu @mbosso_ jina wakati siye aliyeandaa show hii,” amesema Masauti

Hitmaker huyo wa No Stress amesema kuna mwanadada ambaye alimkatiza akiwa jukwaani anatumbuiza jambo ambalo lilimlazimu Willy M Tuva kuingilia kati ndipo akapewa nafasi tena ya kutumbuiza.

“Makosa yatupiwe waandalizi wa show hio mchwara tena sio wote ni dada mmoja tu ambaye singependa nimtaje jina😏Yeye ndo hakutaka kuheshimu kazi yangu na kunionyesha thamani kama msanii wa nyumbani. Lakini kama mpambanaji niliamua kueka kazi kwanza maana sipendi kueka hisia zangu mbele kwakua nina familia nyuma inayoniangalia mimi tu.

Siku ile ya show walienda kinyume na mahitaji yangu kwenye rider lakini wala sikuvunjika moyo kwakua ni kijana ninayepambania sanaa yangu ili familia yangu ipate rizki😣Hakukua ata na usafiri wangu ili kufika sound check,” amesema Masauti .


Hata hivyo amesema mapromota wa tamasha hilo hawakufadhili  usafiri wake kutoka na kwenda kwenye show licha ya kuwa na mkataba wa makubaliano.

Baada ya kama nusu saa hivi, nikiendelea kuperfoem nikaona nyuma kuna mvutano unaendelea kati ya management yangu na watu kwenye stage. Yuleyule dada alitaka kunikatiza show katikati😒Vita hivo viliendelea kati yao na uongozi wangu ambao ulipinga hilo wazo lao la kusmamisha show katikati.

Dj alismamisha show kwasababu yule dada alimtishia kutomlipa🤬 mvutano uliendelea akaja @mzaziwillytuva aliyeingilia kati na kukataa mziki ukatishwe namna hio. Aliungana nasi show ikaendelea. Nikaimba na mashabiki zangu hadi wakati wangu ukaisha ndo nikashuka kwenye stage,” ameeleza Masauti.

Kauli ya masauti inakuja siku chache baada ya Nadia Mukami kufunguka namna ambavyo walidhulumiwa kwenye tamasha la muziki lilofanyika mjini mombasa wikiendi hii iliyopita.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke