Hitmaker wa “Sing’oki”, msanii Masauti amekiri kupata ugumu kumfikia msanii mwenzake Bahati tangu kukamilika kwa uchaguzi mkuu Agosti 9 mwaka huu nchini Kenya.
Masauti amedai Bahati hapokei simu wala hajibu jumbe zake kwenye mtandao wa Instagram, kitendo ambacho kinampa wasi wasi kuhusu hali ya mkali huyo wa ngoma ya “Adhiambo.”
Kauli ya Masauti imekuja mara baada ya moja ya shabiki yake kwenye mtandao wa Instagram kumuuliza kama ana mpango wa kufanya kazi ya pamoja na Bahati.
Utakumbuka Bahati amekuwa kimya tangu apoteze kiti cha ubunge eneo la Mathare kwenye uchaguzi ambao alidai kwamba ulikumbwa na udanganyifu mwingi.