You are currently viewing MASH MWANA AKANUSHA KULELEWA NA MWANAWAKE

MASH MWANA AKANUSHA KULELEWA NA MWANAWAKE

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Mash Mwana amekanusha tuhuma zinazotembea kwenye mitandao ya kijamii kwamba amekuwa akilelewa na mwanamke.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Mash Mwana amesema anawashangaa watu wanavyomsema vibaya mitandaoni kuwa kuna mwanamke anafadhili maisha yake ya kifahari huku akisisitiza kuwa vitu vyote vya kifahari anavyovimiliki ni kutokana na bidii yake.

Hitmaker huyo wa ngoma “Nifungue” amesema wanaoneza uvumi huo mtandaoni wana chuki na mafanikio yake huku akiongeza kuwa kulelewa na mwanamke ni ulimbukeni uliopitiliza hivyo hawezi kufanya vitu kama hivyo.

Kauli yake imekuja mara baada ya watu kudai kuwa gari aina Mercediz Benz aliyozawadiwa kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake alipewa na mwanamke ambaye amekuwa akimlea kwa muda mrefu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke