Mwanamuziki wa Nyimbo za injili nchini Mash mwana ameweka wazi jina la album yake mpya atakayoiachia mwezi Julai mwaka huu.
Katika mahojiano na Spm buzz mash mwana amesema album yake mpya itaitwa “Maajabu the album” na uzinduzi wake utafanyika julai 10 Nairobi Cinema.
Licha ya kutoweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album yake ya Maajabu, mash mwana ametusanua kuwa amewashirikisha wasanii kama Daddy Owen, Irene Robert, Walter Chilambo, Guadian Angel na wengine wengi kusikika kwenye album hiyo.
Maajabu ni album ya kwanza kwa mtu mzima Mash Mwana tangu aanze safari yake ya muziki mwaka wa 2015.