Mwanamuziki wa nyimbo za injili Mash Mwana anaendelea kutupasha mapya kuhusu Album yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia hivi karibuni.
Mkali huyo wa ngoma ya “Nifungue” ametusanua kwamba Album yake mpya imekamilika na itaingia rasmi sokoni Julai 10 mwaka huu.
Licha ya kutoweka wazi jina na nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake hiyo Mash Mwana amewaomba mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea projeect hiyo.
Hii itakuwa ni album ya kwanza kwa mtu mzima Mash Mwana tangu aanze safari yake ya muziki miaka 7 iliyopita.