Huku mashabiki kutoka Kenya wakiendelea kumsifia msanii Nikita Kering baada ya kushinda tuzo mbili zA AFRIMA Best Artist East Africa na Best Group in African RnB & Soul.
Mashabiki wa msaani Zuchu wa WCB wanahisi kuwa Nikita hakustahili kushinda tuzo ya msaani bora wa Afrika Mashariki wa kike.
Kupitia mtandao wa instagram mashabiki hao wamedai kuwa hawajawahi kumsikia na wala hawamfahamu Nikita Kering huku wakidai kuwa Zuchu amekuwa na hit songs nyingi ambazo zimetamba sana Afrika mashariki ikilinganishwa na Nikita.
Ikumbukwe Kenya tulitoka kimasomaso kwenye tuzo za AFRIMA mwaka wa 2021 kupitia Sauti Sol ambao waliibuka washindi kwenye kipingele cha Best group huku msanii chipukizi nchini Shanah Manjeru akishinda kipengele cha Best African Female Artiste.
Wawakilishi wengine kutoka Kenya waliokuwa wanawania tuzo hizo mwaka huu ni pamoja na Nviiri the story teller, Nadia Mukami, Khaligraph Jones, Tanasha donna, Otile Brown, Xeniah Manaseh, na Muthoni the Drummer Queen.