Mashabiki wamemtolea na kumtupia maneno mwanamuziki Nelly kutoka nchini Marekani baada ya stori ya mwanamke mmoja ambaye alipewa shilling 11,388 za kenya kama zawadi baada ya kuokota na kulirudisha begi la Nelly lililokuwa na zaidi ya shilling milllioni 11 za kenya.
Hata hivyo Nelly aliibuka na kukanusha taarifa hiyo kupitia ukurasa wa instagram ambao uliweka video hiyo.
Kwenye uwanja wa comment aliandika hajapoteza begi na wala hafahamu chochote kuhusu begi hilo linaloongelewa kwenye mitandao ya kijamii.