You are currently viewing MASHABIKI WAMVAA REKLESS KWA MADAI YA KUSUSIA SHOW TURKANA

MASHABIKI WAMVAA REKLESS KWA MADAI YA KUSUSIA SHOW TURKANA

Mashabiki wa msanii wa muziki wa gengetone Rekless wameghadhabishwa na hatua ya msanii huyo wa kundi la Ethic Entertainment kukosa kutokea kwenye Onesho la Colour Fest lilofanyika katika hoteli ya kifahari ya Ceamo Village viungani mwa mji wa Lodwar.

Kulingana na mashabiki hao walipigwa na butwaa baada Rekless kushindwa kutokea kwenye onesha la Colour Fest licha waandaji wa tamasha hilo kuwahakikishia kuwa msanii huyo atakuwa moja kati ya wasanii watakaotumbuiza.

Chanzo cha karibu na hoteli ya Ceamo kimesema kuwa baada ya mashabiki kuulizia mbona Rekless hajatokea walitimuliwa na maafisa wa polisi jambo lilowalazimu baadhi ya mashabiki kumtafuta rekless kwa njia ya simu na kumsomea.

Hata hivyo msanii huyo alijitetea kwa kusema kwamba  hawakuelewana na waandaji wa tamasha la colour fest kuhusu ishu ya malipo jambo lilolazimu uongozi wake kuipiga chini shoo hiyo.

Ikumbkwe juzi kati Rekless kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwatangazia mashabiki zake kwamba angetumbuiza katika hoteli ya Ceamo mjini Lodwar Desemba 29 mwaka wa 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke