You are currently viewing MASHABIKI WAVUNJA MAGETI KWA AJILI YA KUMUONA WIZKD O2 ARENA LONDON

MASHABIKI WAVUNJA MAGETI KWA AJILI YA KUMUONA WIZKD O2 ARENA LONDON

Mashabiki waliamua kuvunja vizuizi (barriers) na kuwasukuma walinzi kisha kuingia kwenye ukumbi wa 02 Arena Jijini London Uingereza usiku wa kuamkia leo ambapo nyota kutoka nchini Nigeria Wizkid alikuwa akifanya onesho lake la kwanza kwenye ziara ya Made In Lagos.

Hii imekuja kufuatia mashabiki kuwa na kiu ya kumuona staa huyo ambaye alimaliza tiketi za onesho hilo ndani ya dakika 12 mwezi August mwaka huu. Tiketi za onesho la pili ambalo lilifanyika Novemba 29 pia zilimalizika ndani ya dakika 2 tu tangu ziwekwe mtandaoni.

Waandaaji wa tamasha hilo pamoja na uongozi wa ukumbi huo umesema ulifanikiwa kuwazuia mashabiki ambao walikuwa wakiendelea kuvunja taratibu za uingiaji baada ya wachache kufanikiwa kupenya. Ukumbi huo unabeba jumla ya watu Elfu 20.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke