Msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama amedai mashabiki wake wengi ni wanaume na ndio maana imekuwa vigumu kwake kudumu kwenye mahusiano.
Hata hivyo, tangu amekuwa maarufu kupitia muziki, Maua Sama hajawahi kuweka wazi mahusiano yake licha ya kuandamwa na tetesi za hapa na pale.
“Mashabiki zangu wengi wanaume, ndio maana maboyfriend hawakai, huko kwenu vipi mnavumiliana?,” Maua Sama ameandika Twitter.
Kwa sasa Maua Sama anafanya vizuri na remix ya wimbo wa Mwana FA, Sio Kwa Ubaya