You are currently viewing MASTER J AFUNGUKA SIRI YA MAFANIKIO YA WASANII WA NIGERIA

MASTER J AFUNGUKA SIRI YA MAFANIKIO YA WASANII WA NIGERIA

Mtayarishaji wa muziki BongoFleva, Master J ameeleza sababu za wasanii wa Nigeria kufanya vizuri Afrika na duniani kwa ujumla.

Katika mahojiano yake hivi karibuni amesema kitu ambacho watu hawakifahamu ni kwamba Wanigeria walianza muziki miaka mingi kutokana na maendeleo kwao kutangulia.

“Walianza wakati bado tumelala, hapa tulipo wao walishapita hata miaka 60 iliyopita, kwa hiyo wao kuwa hapa sio kwamba ni bora kuliko sisi bali walianza kitambo wakati sisi hatuna hata TV” amesema.

“Kumbukeni jamani Tanzania TV ilianza mwaka 1994, kuanzia 94 kurudi nyuma huko sisi ni weupe lakini wenzetu hivyo tayari kwao vilikuwepo, hivyo wana uzoefu wa kushindana kimataifa,” amesema Master J.

Ameendelea kwa kusema, “Lakini niwapongeze wasanii wetu kwani kwa muda mfupi spidi ambayo wameenda nayo hadi kina Davido sasa wakiangalia nje wanaona vumbi, kwamba wapo karibu, hiyo ni heshima, hivyo niwapongeze watu ambao wapo kwenye muziki,”

“Kilichobaki wasanii wetu ni kupata connection, kitu ambacho Burna Boy kawazidi hapa nyuma ni connection ya P Diddy tu,” amesema Master J.

Hata hivyo, Master Jay amesisitiza licha ya kuwepo tofauti baina ya wasanii na mashabiki katika muziki wa Bongofleva, ila linapokuja suala la tuzo kubwa za kimataifa umoja unatakiwa kwa sababu Wanigeria ndipo wamefanikiwa zaidi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke