Staa wa muziki wa Bongo Fleva Maua Sama ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zai” amewabarki mashabiki zake na “Cinema EP” ambayo ina jumla ya nyimbo 7 za moto, ikiwa na kolabo 2 pekee kutoka kwa wakali kama Ali Kiba na Jux.
EP hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani ina ngoma kama Nioneshe, Fallingi in Love, Tomorow, Namwachia, Vimba, Nimeridhia, na Never Ever.
Hii ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Maua Sama, tangu aanze safari yake ya muziki mwaka wa 2015.