Baada ya kuwa na muendelezo mzuri wa kuachia ngoma back to back ambapo tayari ana mwezi mmoja tangu aachie smash hit yake ya ‘Zai’, Maua Sama ana kazi nyingine mpya ambayo ni ‘Baba Jeni’, na kupitia taarifa yake kwa umma ameeleza kwanini anaachia kazi hivyo.
Msanii huyo amebainisha kuwa hiyo ni staili tu ya kutoa muziki wake ambayo ameipa jina la “Uzazi wa mpango wa muziki” yaani mtoto akienda mjini anamleta mwengine, huku akiwataka mashabiki waendelee kuwa wavumilivu.
Hata hivyo ngoma hizo ambazo Maua sama amekuwa akiachia siku za hivi karibuni zimekuwa zikifanya vizuri sana.
Ikumbukwe Maua Sama ni miongoni mwa wasanii wakike wanaofanya vizuri nchini Tanzania tangu alipoibuka miaka minne iliyopita akiwa na mkali wa rap Mwana f.a ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Muheza mkoani Tanga.