MAUA SAMA AMJIBU ZUCHU KIMTINDO

Mwanamuziki wa Bongofleva, Maua Sama amewataka wasanii wenzake kuacha kupeana shinikizo zisizo kuwa na msingi kwenye masuala ya muziki.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Hitmaker huyo wa “ZAI” ameandika ujumbe unaosomeka “Wasanii tupunguze mikwara tutauana kwa pressur” na kumalizia na emoji ya kicheko.

Ujumbe huo wa Maua Sama umetafsiriwa na walimwengu kuwa ni vijembe kwenda kwa Zuchu ambaye alidai kuwa kwa uandishi wake anafaa kuwekwa kwenye ligi ya wasanii wa kiume maana kina dada atawaonea.

Utakumbuka kwa sasa Maua Sama anaendelea kufanya vizuri na Extended Playlist (EP) yake iitwayo “CINEMA” yenye jumla ya nyimbo saba za moto ambazo amewashirikisha wasanii wawili, Alikiba na Jux.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke