Hakika huu ni mwaka wenye neema kwa msanii Maua Sama kwasababu licha ya ngoma zake kufanya vizuri kupitia digital platforms mbalimbali, kubwa zaidi ni kuwa miongoni mwa watakaowania kwenye tuzo za nchini Uholanzi.
Maua ametajwa kuwania tuzo ya video bora ya mwaka kupitia video ya ZAI kwenye tuzo za “New Vision International Awards” (NVIFF) huko Amsterdam nchini Uholanzi.
Video hiyo ya Zai ambayo ina mwezi mmoja tangu ipandishwe Youtube, hadi sasa ina zaidi ya views 796K kwenye chaneli rasmi ya Maua Sama.
Tuzo hizo za nchini Uholanzi zinatarajiwa kutolewa Desemba 20, 2021.