Huenda tukio la Harmonize kumvisha Kajala pete ya uchumba limemgusa pakubwa mwimbaji wa bongofleva maua sama akitamani kuwa kwenye mahusiano, kwani ametangaza kuwa yupo single.
Maua ametumia neno “Jimbo Lipo Wazi” akiwa na maana kwamba hayupo kwenye mahusiano kama ambavyo ujumbe huo unavyomaanisha huko mitaani.
Maua sama ameandika “JIMBO LIPO WAZI ” akiwa ameambatanisha na emoji ya pete pamoja na pilipili.
Hata hivyo kwenye post hiyo ya maua sama upande wa comments, mashabiki wake wanaonekana kutokubaliana nae kwa hilo wakiamini yupo mwenye jimbo lake.