You are currently viewing MAUA SAMA AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA

MAUA SAMA AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA

Mwimbaji nyota wa muziki wa Bongofleva, msanii Maua Sama amewaacha njia panda mashabiki wake kufuatia kuchapisha ujumbe unaoshiria yupo mbioni kuachia EP au Minitape.

Katika post yake kwenye mtandao wa Instagram Maua Sama ametangaza kutengeneza wimbo mrefu sana wenye dakika 23, verse 14 na chorus 5.

Maua Sama ambaye anajiita Maua Kobe ameeleza katika hizo dakika 23 amekata dakika 7 na amepata video 4.

Hata hivyo amesema kuna verse mbili ambazo zimefanywa na wasanii wa kiume na kwa upande wa Beat wamehusika wataarishaji wane huku akiwahakikishia mashabiki zake kuwa wimbo huo utakuwa Ni mzuri.

“Nimeamua kutengeneza wimbo mmoja mrefu sana. Una dakika 23, verse 14, chorus 5. Verse 2 wamefanya kaka zangu, beat imetengenezwa na watayarishaji 4”. Ameeleza Maua.

“Nimekata dakika 7 nimepata video 4, ni muziki mzuri sana! Niamini mimi” aliongeza mauasama. “Weka HESHIMA kwenye jina langu”.Ameandika kupitia instastory yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke