You are currently viewing MAUNDA NZORO AFARIKI AKITOKEA MSIBANI USIKU WA KUAMKIA LEO

MAUNDA NZORO AFARIKI AKITOKEA MSIBANI USIKU WA KUAMKIA LEO

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maunda Zorro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo April 14, 2022 kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Banana Zorro ambaye ni kaka wa marehemu, mdogo wake alifariki kufuatia ajali ya gari iliyotokea saa chache baada ya kuachana naye.

Banana ameeleza kuwa aliachana na Maunda saa 12 jioni baada ya kujumuika kwenye msiba wa rafiki yao wa muda mrefu.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa gari alilokuwa akiendesha Maunda liligongana na lori la mchanga na kusababisha umauti wake.

Maunda kutoka katika familia ya waimbaji ya Mzee Zahir Zorro amewaacha watoto watatu na atakumbukwa kwa nyimbo mbalimbali alizoshiriki ikiwemo ‘Nataka niwe wako’ na Mapenzi ni ya wawili’.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke