You are currently viewing MAURICE KIRYA ATANGAZA KUWANIA URAIS WA MUUNGANO WA WANAMUZIKI UGANDA

MAURICE KIRYA ATANGAZA KUWANIA URAIS WA MUUNGANO WA WANAMUZIKI UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini uganda Maurice Kirya ametia nia ya kugombea  wadhfa wa urais katika muungano wa wanamuziki nchini humo kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni.

Kirya amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa kusema kwamba amepokea maombi mengi kutoka wasanii wenzake pamoja na mashabiki, kugombea urais wa muungano huo kutokana na uelewa mpana ambao ako nao juu ya tasnia ya muziki nchini uganda.

Msanii huyo amesema ana vigezo vyote vya kuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda huku akisisitiza kuwa lengo lake kuu ni kuwaunganisha wasanii na kuboresha kiwanda cha muziki nchini uganda kutokana na ujuzi ambao ameupata kwenye muziki wake

Kauli ya Maurice Kirya imekuja mara baada ya msanii bebe cool kumtaka kuungana na wasanii Cindy Sanyu, Daddy Andre, na King Saha ambao tayari ametangaza kuwania kinyanganyiro cha urais wa muungano wa wasanii nchini uganda kwenye uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke