You are currently viewing MAURICE KIRYA AWAPA SOMO WASANII WAMBEA NCHINI UGANDA.

MAURICE KIRYA AWAPA SOMO WASANII WAMBEA NCHINI UGANDA.

Mwanamuziki kutoka Uganda Maurice Kirya amewapa somo baadhi ya wasanii wakubwa ambao wamekuwa na tabia ya kuwachamba au kuwazungumzia vibaya wasanii wenzao wakiwa kwenye shughuli zao za kimuziki.

Kupitia mitandao yake kijamii Kirya ambaye ameonekana kukerwa na vitendo hivyo amesema kuna baadhi ya wasanii wakubwa nchini uganda ambao hutumia muda wao mwingi kuwasegenya na kuwakatisha tamaa wasanii wenzao badala ya kwenda studio kuboresha kazi zao za muziki.

“Some of the most talented artists I know in Uganda spend most of their time gossiping about other artists and how they think they are better than them, Instead of getting in the studio and putting their talent to work,” Ameandika kwenye mitandao yake ya kijamii.

Msanii huyo amewataka wasanii wanaoendeleza kasumba ya kuwasimanga wasanii wenzao kukoma mara moja na badala yake waelekeze nguvu zao kwenye suala la kutoa muziki mzuri.

“So this goes out to you talented artists, if you think you’re good, stop trying to discourage artists that are actually doing the work and putting it out there. They are brave, and they’re following their dreams,”  Ameongeza.

Utakumbuka miezi kadhaa iliyopita Mwandishi wa nyimbo na prodyuza Nince Henry alijitokeza na kudai kuwa kuna baadhi ya wasanii nchini Uganda wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina ili wabaki kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke