You are currently viewing MAURICE KIRYA MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

MAURICE KIRYA MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Nyota wa muziki nchini uganda Maurice Kirya ameweka wazi jina la album yake mpya ambayo ana mpango kuachia ndani ya mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Maurice Kirya amesema album hiyo ameipa jina la The Road to Kirya  na itaingia sokoni Mei 6 mwaka 2022.

Msanii huyo Amesema amewekeza pesa nyingi kuiandaa album hiyo ambayo kwa mujibu wake ni moja kati ya album ghali kutayarishwa na msanii wa afrika kwani ina muziki wa kitofauti sana ambao ni wasanii wachache hufanya barani afrika.

Hii itakuwa ni Album ya 6 kwa mtu mzima Maurice Kirya,  tangu aanze safari yake ya muziki na itangumzia changamoto alizokutana nazo kwenye muziki wake

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke