You are currently viewing MAUZO YA MUZIKI WA R.KELLY WAPANDA KWA ASILIMIA 500 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA

MAUZO YA MUZIKI WA R.KELLY WAPANDA KWA ASILIMIA 500 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA

Mauzo ya muziki wa R. Kelly yameripotiwa kupanda kwa asilimia 517 tangu akutwe na hatia ya mashtaka ya unyanyasaji wa kingono na mengine.

Kwa mujibu wa Rolling Stone, mauzo ya muziki wake kwenye majukwaa ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni (Digital Platforms) yamepanda kutoka millioni 11.2 hadi millioni 13.3 ikiwa ni wiki moja tangu akutwe na hatia ambayo huwenda ikampeleka gerezani miaka 10 au hata kifungo cha maisha.

Mitandao kama Apple Music na Spotify ilizima muziki wa R. Kelly, huku wasanii kama Chance the Rapper, Lady Gaga, Ciara na Celine Dion walimfuta kwenye Kolabo za nyimbo ambazo walifanya naye.

Mwishoni mwa Wiki iliyopita YouTube ilizifungia akaunti zake mbili za muziki kwenye mtandao huo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke