Hitmaker wa “Moyo”, Msanii Mbosso amefunguka uhusiano wake na Bosi wa Next Level Music Rayvanny.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Mbosso amesema licha ya Rayvanny kuondoka kwenye lebo ya WCB bado wana uwezo wa kufanya kazi pamoja kwani wao ni marafiki wakubwa.
“Ni mwanangu, kwa hiyo inapokuja kazi ambayo natakiwa nifanye na Rayvanny lazima tufanye ni rafiki yangu, nakutana naye, anakuja ofisini tunapiga stori, yaani hakuna noma,” amesema Mbosso.
Julai mwaka huu Rayvanny alijiondoa rasmi kwenye lebo ya WCB aliyoitumikia kwa miaka saba na kuelekeza nguvu zake katika lebo yake, Next Level Music ambayo inamsimamia msanii Mac Voice.
Utakumbuka chini ya WCB Mbosso alimshirikisha Rayvanny katika wimbo wake uitwao Pakua kutoka kwenye albamu yake, Definition of Love huku Rayvanny akimshirikisha Mbosso kwenye ngoma yake, Zuena inayopatika kwenye albamu, Sound From Africa.