Msanii wa Bongo Fleva, Mbosso amefunguka kuhusu tatizo la ugonjwa wa moyo ambalo limemwandama tangu akiwa mtoto.
Akizungumza katika mahojiano maalum Mbosso ambaye ni msanii wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) amesema kwamba ugonjwa huo unasababishwa na mafuta kuwa mengi kwenye mishipa ya damu ya kwenda kwenye moyo.
Dalili alilozitaja za ugonjwa huo ni pamoja na maumivu upande wa kushoto wa kifua, viungo kupoteza hisia na kwake anatetemeka vidole.
Hata hivyo Mbosso amesema tangu atambue kuwa ana ugonjwa huo wa moyo amekuwa akimtembelea daktari wake mara kwa mara na kuyafuata maagizo yake katika juhudi za kutaka kupo.