You are currently viewing Mbosso atangaza ujio wa ziara yake ya muziki nchini Marekani

Mbosso atangaza ujio wa ziara yake ya muziki nchini Marekani

Mwimbaji nyota kutoka lebo ya WCB, Mbosso ametangaza rasmi ujio wa ziara yake kimuziki ya kimatifa ya Marekani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema ziara hiyo itaanza rasmi tarehe 25, mwezi Novemba hadi 16, mwezi Desemba.

“King Khan Live in USA: Nov 25th – Dec 16th.”, Amaandika Mbosso.

Mbosso ambaye ana zaidi ya streams Milioni 100 katika mtandao wa Boomplay, kwenye mahojiano yake na Dizzim Online mwishoni mwa wikiendi hii iliyoputa, aliweka wazi Oktoba 21, anaachia EP yake mpya ambayo ameitaja kuwa ndio project yake atakayoifungia mwaka.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke