You are currently viewing MBUZI GANG: KIBURI IMEWAPONZA WASANII WA GENGETONE

MBUZI GANG: KIBURI IMEWAPONZA WASANII WA GENGETONE

Wasanii wa kundi la Mbuzi Gang wamefunguka na kudai kwamba kiburi ndio imewaponza baadhi ya wasanii wa Gengetone.

Katika mahojiano yao hivi karibuni wamesema baadhi ya wasanii wa muziki huo wameanza kulaza damu kutokana na kupata views nyingi kwenye mtandao wa youtube jambo ambalo limewapelekea kuingiwa na kiburi na kujiona ni wakubwa zaidi kuliko wasanii wenzao.

Aidha wamepuzilia mbali madai kuwa muziki wa Gengetone umepitwa na wakati kwa kusema kuwa dhana hiyo imetokana na ukosefu wa ushirikiano miongoni mwa wasanii wa muziki huo.

Katika hatua nyingine wamekanusha tuhuma zilizoibuliwa na baaadhi ya wasanii wa Gengetone kwamba lebo za muziki zinawanyanyasa huku wakisema kuwa wasanii hao ndio wakulaumiwa kwani wamekwenda kinyume na mikataba ya lebo wanazofanya kazi nazo kwa kutoachia nyimbo.

Hata hivyo wamewataka wasanii wa Gengetone waache uvivu kwa kulalamika kuwa wanaporwa pesa zao na badala yake watie bidii kwenye shughuli zao za muziki ili waweze kupata riziki itakayowasaidia maishani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke