You are currently viewing MBUZI GANG WAJIBU SUALA LA NYIMBO ZAO KUFANANA

MBUZI GANG WAJIBU SUALA LA NYIMBO ZAO KUFANANA

Wasanii wa kundi la Mbuzi Gang wamewajibu wale wanaosema kuwa nyimbo zao zinafanana.

Katika mahojiano yao ya hivi karibuni wamesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa wamekuwa wakiachia nyimbo zenye melodies tofauti zinazoenda na nyakati zilizopo.

Wakali hao wa ngoma ya shamra shamra Wamesema wanaodai nyimbo zao zinafanana wanaowaona wivu kutokana na mafanikio ambayo wanayapata kwenye muziki wao huku wakisisitiza kuwa wataendelea kutoa muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki zao.

Kauli yao imekuja mara baada ya watu kudai kuwa tangu wapate umaarufu kupitia wimbo wao wa “Shamra Shamra” wamekuwa wakiachia nyimbo zenye melodies zinazofanana na wimbo huo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke