Kama kuna kitu ambacho Mchekeshaji Eric Omondi anajivunia kuwa nacho ni kujiamini, baada ya jaribio lake la kwanza la kuikingia kifua muziki wa kenya kutibuka mwaka jana na hata kupelekea kukamatwa kwake, mchekeshaji huyo amerudi tena bungeni kushinikiza mswada kutaka muziki wa Kenya upewe hadhi ujadiliwe.
Akizungumza nje ya majengo ya bunge Omondi amesema hatelekeza msimamo wake wa kutaka asilimia 75 ya muziki wa Kenya upigwe kwenye vituo vya redio na runinga nchini hadi pale mswaada huo itapitisha kuwa sheria bungeni.
Hata hivyo wabunge John Kiarie na David Ole Sankok wameonekana kumuunga mkongo eric omondi katika harakati zake za kupigania maslahi ya wasanii wa Kenya huku wakihapa kwa kauli moja kuhakikisha mswada huo unapitishwa bungeni