You are currently viewing MCHEKESHAJI KENDRICK MULAMWAH AGEUKIA MUZIKI WA HIPHOP

MCHEKESHAJI KENDRICK MULAMWAH AGEUKIA MUZIKI WA HIPHOP

Mchekeshaji maarufu nchini Kendrick Mulamwah ameamua kugeukia muziki wa Hiphop ikiwa ni katika kutimiza ndoto zake za kuwa rapa.

Mulamwah ambaye ametamba kwenye fani ya ucheshi kwa miaka mingi ameachia rasmi wimbo wake wa kwanza wenye mahadhi ya HipHop ambao kaupa jina la “The Recoil Freestyle”.

Kuptia ngoma hiyo ambayo ni disstrack, mchekeshaji huyo amesikika akiwachana watu wote ambao wamekuwa wakimubeza kupitia kazi zake za ucheshi mara baada ya kuachana na Baby Mama wake Carol ‘Sonnie’ Muthoni.

Hata hivyo ngoma hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kumkatisha tamaa asigeukia muziki kwani hana kipaji cha kurap huku wengine wakimpongeza kwa hatua ya kuonesha upande wake mwingine kando na ucheshi.

Mulamwah anajiunga kwenye orodha ya mastaa kama Prof. Harmo, na Flaqo ambao hapo awali walitambulika kama wasanii wa ucheshi na baadae wakageukia kufanya muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke