You are currently viewing MCHEKESHAJI OGA OBINNA AZUA GUMZO MTANDAONI

MCHEKESHAJI OGA OBINNA AZUA GUMZO MTANDAONI

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya Oga Obinna amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kutoa kauli kuwa wanawake waliochora tattoo na kutoboa miili yao kwa kuweka vipini kwenye pua sio wife material.

Kauli hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakisema kuwa hayupo sahihi ikizingatiwa kuwa kila mwanamke ana haki ya kuolewa kwani tattoo na vipini ni urembo tu wa nje na sio tabia.

Moja ya wadau kutoka Twitter anasema “yote inategemea kile unachotaka. ukimpenda kwa kutoboa na tattoo zake basi utamuoa. wakati mwingine huhitaji kuangalia mambo kama hayo,mwanamke anaweza kuwa na tattoo na akawa mama bora kwa watoto na familia yake”.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke