Mchekeshaji wa YY ameomba msamaha kwa kutania kiasi cha pesa ambacho mwanamuziki wa Kenya Kenrazy anatoza kwenye shows zake.
Katika mahojiano na Plug TV, YY alinukuliwa akisema kuwa hawezimudu gharama za kumualika msanii Willy Paul kwenye shows zake kwa kuwa anatoza pesa nyingi ambapo alienda mbali Zaidi na kutania kuwa ni heri ampe show timmy tdat pamoja na kenrazy kwa sababu wasanii hao hawahitaji pesa nyingi kutumbuiza kwenye shows.
“Kama tusipokuafford, tutaita Timmy Tdat na atakuja Hadi na Kenrazy na 40k.” Alisema.
Kauli hiyo ilionekena kumkera kenrazy ambaye alitumia ukurasa wake wa instagram kusema kwamba yy alimvunjia heshima kwa kuidharau na kuishusha brand yake ya muziki ambayo ametengeneza kwa muda na pia ni brand ambayo imekuwa ikimuingiza kipato ambacho kimemsaidia kukithi mahitaji ya familia yake.
“Nimekuwa nikijitahidi sana kutengeneza chapa yangu kila siku na hivyo siwezi kubali kauli kama hiyo inayotoka kwa mtu kama wewe. Kwa kweli umenikosea sana, nilidhani unanijua vizuri zaidi. Unaniona nafanya kazi kila siku bila faida yeyote kutoka kwenye tasnia hii na kulea familia yangu kwa miaka hiyo yote, hivyo kukejeli sana yangu ni jambo lisilokubalika.”, Kenrazy aliandika kwa masikitiko.
Hata hivyo Comedian YY alilazimika kumuomba radhi msanii kenrazy kwa kusema kwamba anasikitika kumtania Kenrazy na kumfanya ajisikie vibaya, kwani hakuwa na nia ya kujeli brand au chapa yake ikizingatiwa kuwa ni msanii mkubwa ambaye ameacha alama kwenye muziki wa Kenya.