Mchezo wa nusu fainali ya Carabao Cup, kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal umesogezwa mbele, sababu kubwa ikiwa ni maambukizi ya Virusi vya Corona.
Mchezo huo uliokuwa upigwe kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Anfield sasa utapigwa Januari 13 kisha marudio ni Januari 20, mwaka wa 2022.
Liverpool chini ya Kocha Jurgen Klopp iliomba mchezo huo kusogezwa mbele kutokana na msaidizi wa kocha huyo, Pep Lijnders na wachezaji wengike kadhaa kuoata maambukizi ya Virusi vya Corona.