Mchumba wa msanii Harmonize, Kajala Masanja amewafunga midomo walimwengu mara baada ya kuthibitisha kuwa ana ujauzito wa Bosi wa Konde Gang.
Kupitia instastory yake ameposti kipande cha video akilishika tumbo lake linaloonekana ni mjamzito na kuandika; “I can’t wait…” ujumbe ambao umewaaminisha mashabiki kuwa kweli ni mjamzito.
Hata hivyo wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wamepinga taarifa hiyo huku wakihoji kuwa sio tumbo la Kajala ambalo linaonekana kwenye video hiyo bali inaweza ikawa ni Ujauzito wa mtu wao wa Karibu.