You are currently viewing MCHUMBA WA STIVO THE SIMPLE BOY AANIKA MAOVU AMBAYO MSANII HUYO ANAPITIA CHINI UONGOZI WAKE WA MADE IN KIBERA

MCHUMBA WA STIVO THE SIMPLE BOY AANIKA MAOVU AMBAYO MSANII HUYO ANAPITIA CHINI UONGOZI WAKE WA MADE IN KIBERA

Mpenzi wa msanii Stivo the Simple boy Pritty Vishy ameanika maovu ambayo msanii huyo amekuwa akipitia chini ya uongozi wake wa Made in Kibera.

Akipiga stori na SPM Buzz mrembo huyo amesema uongozi wa Stivo umekuwa ukipora miraba ya nyimbo za msanii huyo huku akitoa mfano kuna kipindi stivo alisaini dili la shillingi laki 2 lakini uongozi wake ulimlipa shillingi elfu 4.

Pritty Vishy ameenda mbali zaidi na kusema kuwa uongozi wa stivo umekuwa ukidhibiti mitandao yote ya kijamii ya msanii huyo baada ya video akiwa na stivo katika mazingira mabaya kuenea mtandaoni.

Hata hivyo amesema stivo amekata mawasiliano nae baada kuhama Kibera huku akiongeza kuwa uamuzi huo umetokana na video iliyosambaa kwenye mtandao wa Tiktok ambayo uongozi wake haukupendezwa nayo.

Hii sio mara ya kwanza kwa stivo the simple kudaiwa kuwa anapitia maisha magumu chini uongozi wake wa made in kibera mwaka jana watumiaji wa mitandao ya kijamii waliibua madai hayo jambo lilofanya uongozi wake  kujitokeza na kukana tuhuma hizo.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke