You are currently viewing MEEK MILL AIBWATUKIA LEBO YAKE,ADAI KUTOLIPWA PESA ZAKE.

MEEK MILL AIBWATUKIA LEBO YAKE,ADAI KUTOLIPWA PESA ZAKE.

Rapa kutoka nchini Marekani, Meek Mill ameamua kuichana Lebo yake kwa kile anachodai kwamba haijamlipa pesa zake zilizotokana na muziki wake kuuzwa.

Kupitia mfululizo wa tweets zake  kwenye mtandao wa Twitter Meek Mill amesema hajalipwa na hafahamu ni kiasi gani cha pesa lebo yake imeingiza kutoka kwenye muziki wake ambapo ameenda  mbali zaidi na kusema kwamba anahitaji Mwanasheria wa kumtetea ili aweze kupata haki yake.

Hakuishia hapo, Meek Mill ametishia kuanika wazi mkataba wake ifikapo Jumatatu ijayo ili dunia ione udhalimu wa lebo yake.

Hata hivyo Meek Mill ambaye anasimamiwa na Roc Nation, hajaweka wazi jina la Label ambayo anaituhumu, kama ni Maybach Music Group au Atlantic Records

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke