Rapa kutoka nchini Marekani Meek Mill anarudisha fadhila kwao, tovuti ya TMZ imeripoti kwamba rapa huyo atatumia zaidi ya shillingi milllioni 56.7 za Kenya kwa ajili ya kutoa zawadi pamoja na mahitaji mengine mbali mbali kwa familia zenye uhitaji mjini kwao Philadelphia msimu huu wa Sikukuu.
Meek Mill ambaye alizaliwa na kukulia Philadelphia amepanga kutoa zawadi kibao zikiwemo Pikipiki, Video game gift cards, Laptops, tablets, midoli na zawadi nyingine kibao. Aidha imeelezwa kwamba atasindikizwa na washirika wake wakubwa; Robert Kraft na Michael Rubin pia mameneja wake toka Roc Nation.