You are currently viewing MEGAN THEE STALLION AAELEZA KWA UCHUNGU ALIVYOPIGWA RISASI NA TORY LANEZ

MEGAN THEE STALLION AAELEZA KWA UCHUNGU ALIVYOPIGWA RISASI NA TORY LANEZ

Rapa kutoka Marekani Megan Thee Stallion ameendelea kufunguka ambayo hatuyafahamu kwenye shtaka lake la kupigwa risasi ya mguu na Tory Lanez Julai 12 mwaka 2020 Jijini Los Angeles.

Televisheni ya CBS imeachia mahojiano yote ya Megan Thee Stallion ambapo mrembo huyo amesikika kwamba Tory Lanez alijaribu kumuonga na shilling million 115 za kenya ili asiwaambie polisi kuwa ndiye aliyempiga risasi.

“Aliomba radhi, alisema samahani sana tafadhali usimwambie mtu yeyote, nitakupatia ‘Dola Milioni’ kama hutosema chochote.” alieleza Megan Thee Stallion kwa uchungu huku akifuta machozi.

Aprili 6 mwaka huu Tory Lanez aliachiwa kwa dhamana ya shilling milllioni 40 za Kenya baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka amri ya mahakama iliyotolewa kumkinga Megan Thee stallion kwenye shtaka lao linaloendelea.

Ikumbukwe Tory Lanez anakabiliwa na Mashtaka mawili ambayo ni kumshambulia rapa Megan thee Stallion mwaka 2020 na pia kubeba silaha yenye risasi kinyume na sheria.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke