You are currently viewing MEGAN THEE STALLION ALAMBA DILI LA USHIRIKIANO NA KAMPUNI YA NETFLIX

MEGAN THEE STALLION ALAMBA DILI LA USHIRIKIANO NA KAMPUNI YA NETFLIX

Rapa wa kike kutoka nchini Marekani Megan Thee Stallion ametangaza kusaini dili nono la ushirikiano na kampuni ya Netflix.

Megan Thee Stallion amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “Siku zote nimekuwa na hamu ya kusimulia hadithi za kibunifu na za kuburudisha, hivyo nimefurahishwa sana na ushirikiano huu na Netflix. Kujitupa kwenye utayarishaji ni hatua inayofuata kwenye safari yangu kama mjasiriamali na nashindwa kusubiri kuleta mawazo yangu kwenye uhai ili nanyi mtazame.”

Dili hilo litamuwezesha rapa huyo kubuni na kutengeneza maudhui ikiwemo series na miradi mingine kwa ajili ya Netflix.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke