Msanii wa singeli nchini Tanzania Meja Kunta amefunguka sababu za kuwa na urafiki mkubwa na wachezaji wa mpira wa miguu kuliko wasanii wenzie.
Akijibu swali la shabiki yake kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema watu wa mpira wako bize na mishe zao ila wasanii akikaa nao sana ni wanafi ki.
Katika hatua nyingine ameweka wazi kuwa kwa sasa hayupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake Cappuccino Tunda
Ikumbukwe meja kunta na Cappuccino Tunda walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi hadi kufikia hatua ya kuvalishana pete ya uchumba.