Staa wa muziki nchini Mejja amefunguka kuwa hatokuja kuweka wazi mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni hitmaker huyo wa “Kanairo Dating” amesema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu mahusiano yake ya nyuma yalikumbwa na mikosi kutokana yeye kuanika mtandaoni.
Mejja ambaye amethibitisha kuwa kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi amesema hana mpango wa kumchumbia mtu maarufu hasa msanii mwenzake kwani mastaa wengi huwa hayadumu kwenye mahusiano.
Utakumbuka Mejja alikuwa kwenye mahusiano na mrembo aitwaye Milly Wairimu lakini walikuja wakaachana kwa madai ya usaliti.