Msanii nyota nchini Mejja amekanusha madai yanayotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa amerudiana na baby mama wake Milly Wairimu.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Mejja amesema madai hayo haya msingi wowote ikizingatiwa kuwa ameyasahau mambo yote yaliyotokea kati yake na mke wake huyo.
Kauli ya Mejja inakuja siku chache baada ya Milly Wairimu kudai kuwa Mejja alimtelekeza walipokuwa wanachumbiana. Mrembo huyo alienda mbali zaidi na kuahidi kuaanika kilichopelekea mahusiano yake na mwanamuziki huyo kuingiwa na dosari.